BurudaniVideos

Msechu kutuwakilisha TPF

Mshiriki Peter Msechu amekuwa mmoja kati ya washiriki watano kutoka Tanzania waliochaguliwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya kupata mkataba katika shindano la kusaka vipaji vya muziki katika ukanda wa Afrika Masahariki Tusker Project Fame kwa mwaka 2010. [Exclusive Video]

Peter Msechu anakumbukwa zaidi kwa kuwa mmoja wa washiriki wa Bongo Star Search kwa mwaka jana  ambapo alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda kabla na kuibuka na kuwa mshindi wa pili katika fainali zilizofanyika Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari ambazo zimetufikia sasa hivi watanzania hao watano watajiunga na washiriki wenzao kumi na mbili kutoka katika nchi zingine nne za Afrika mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan ya Kusini.

{hwdvs-player}id=1152|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Peter Msechu pamoja na wenzake wanne wamepatikana baada ya kushiriki usaili wa kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita wamepatikana baada ya jopo la majaji na waandaaji kuwapitisha katika mchujo ulioshirikisha zaidi ya washiriki mia arobaini.

Akiwataja washiriki hao msemaji mkuu wa kampuni ya bia ya Serengeti bibie Teddy Mapunda aliyataja majina hayo kuwa ni pamoja na Janeth Audax Christopher,Aneth S. Kushaba, Leah M. Mwambogela, Cynthia Bavo na Peter J. Msechu.

Washiriki hao wa tano kutoka nchini Tanzania wanatarajiwa kupanda ndege alfajiri ya kesho kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya ambapo wanaingia kambini katika academy ya Tusker Project Fame siku ya jumamosi  ya wikiendi hii.

Shindano hilo ambalo linadhaminiwa na bia ya Tusker ambayo kwa sasa inzalishwa nchini Tanzania na kampuni ya bia Serengeti katika ubia na kampuni ya bia ya Afrika Mashariki EABL.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents