Michezo

Mshambuliaji hatari wa Ruvu Shooting avitoa udenda vilabu vya Simba na Yanga

By  | 

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Ruvu Shooting Abdulrahman Mussa, amefungua milango kwa klabu za Simba, Yanga na Azam FC kwa kuzitaka kufuata utaratibu wa mazungumzo kwani yeye yupo tayari kuihama klabu yake.

Abdulrahman Mussa amefungua Milango kwa Vogogo wa VPL

Abdulrahman Mussa

Abdulrahman ambaye kwa sasa ameshaifungia Ruvu Shooting mabao 13 na ndiye mchezaji bora kwa mwezi Aprili, amesema shughuli yake ni kucheza soka na linapokuja suala la kutakiwa na klabu yoyote kati ya Simba, Yanga au Azam FC hana kipingamizi cha kuwaacha maafande wa jeshi la kujenga taifa, Ruvu Shootimg.

Mkataba wangu unaisha msimu huu na niwaambie tu, viongozi wa klabu za Simba, Yanga na Azam FC waje tuzungumze ili tupate muafaka ambao utanisaidia kujua ni wapi nitakapoangukia msimu ujao” Alisema Abdulrahman kwenye mahojiano yake na Dar 24.

Kwa upande mwingine, Abdulrahman amekiri wazi kuwa, bado hajafanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting ili kuangalia uwezekano wa kusaini mkataba mpya, lakini bado amesisitiza yupo tayari kuondoka endapo klabu za Simba, Yanga na Azam FC zitakua tayari kumsajili.

Tetesi zinadai vilabu vya Yanga na Simba ambavyo vimepata mabilioni kwa kusaini mkataba wa udhamini na Kampuni ya Kubashiri ya SportPesa vinapigana vikumbo kumnasa mchezaji huyo mwenye magoli 13 kwa msimu huu.

By Godfrey Mgallah

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments