Habari

Msondo yapata makao makuu Mbagala

Msondo Ngoma BandBENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania Msondo Ngoma Music, ‘Mambo Hadharani Discipline’ imepata ukumbi mpya ulioko Mbagala, Temeke jijini Dar es Salaam ambao hivi sasa ndio utakuwa makao makuu ya bendi hiyo.



na Abdallah Menssah


BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania Msondo Ngoma Music, ‘Mambo Hadharani Discipline’ imepata ukumbi mpya ulioko Mbagala, Temeke jijini Dar es Salaam ambao hivi sasa ndio utakuwa makao makuu ya bendi hiyo.


Mmoja wa viongozi wa bendi hiyo, Saidi Mabera aliliambia gazeti hili juzi, kuwa ukumbi huo ambao zamani ulikuwa ukijulikana kama Kwetu Bar, ndio sasa utakuwa makao makuu ya bendi hiyo kutoka Amana Social Hall, Ilala jijini.


Mabera alisema, kuwa watakuwa wakiutumia ukumbi huo, kama kitega uchumi cha nendi hiyo kwa kuukodisha kwa makundi mengine mbalimbali ya muziki yatakayokuwa yakihitaji huduma za ukumbi huo ambao sasa utaanza kujulikana kwa jina la Msondo Ngoma Club.


Aidha, kiongozi huyo aliongeza kuwa uongozi umekaa na kukubaliana kuukarabati upya ukumbi huo ili kuubadilisha na kuupa sura ya kibiashara sambamba na hadhi ya kisasa, ambako utakapokwisha kukamilika, bendo hiyo itakuwa ikitumbuiza kila za Jumamosi.


Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents