Habari

Mtoto wa Sylvester Stallone, Sage Stallone afariki dunia.

Mtoto wa muigizaji maarufu wa filamu za action Sylvester Stallone aitwaye Sage Stallone, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 36 kutokana na drug overdose (matumizi ya madawa ya kulevya yaliyopitiliza).
Sage alikutwa amefariki kwenye nyumba yake ya jijini Los Angeles.
Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, taarifa zaidi kuhusiana na kifo chake hazijawa na uhakika sana.
Sage alikutwa kwenye nyumba yake na mfanyakazi wake ama mpenzi wake, kwa mujibu wa TMZ.
Kutokana na kukutwa hivyo iliitwa ambulance nyumbani kwake na madaktari kumtangaza kuwa amefariki.
Msemaji wa Sylvester Stallone,Michelle Bega ameiambia TMZ kuwa “Sylvester Stallone amehuzunishwa vibaya na kifo cha ghafla cha mwanae Sage Stallone.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents