Burudani

Muda utaongea iwapo nitashindwa au nitaweza kumrudisha Lord Eyez – Barakah Da Prince

Uamuzi wa Barakah The Prince kumsainisha Lord Eyez kwenye label yake mpya aliyoianzisha, umepokelewa kwa hisia tofauti. Rapper Bonta aliambia Bongo5 kuwa ni aibu kwenye hip pop.

Na sasa Barakah ameijibu kauli ya member huyo mwingine wa Weusi huku akidai kuwa ni mapema kwa sasa watu kujudge iwapo atafeli kumrudisha rapper huyo na kwamba watu hawajui mipango yake ikoje.

“Sidhani kama huwa kuna aibu kwenye biashara,” Barakah amemuambia mtangazaji wa ABM Radio ya Dodoma, DJ Rodger. “Mtu ukiwa unapanga suala lako sometimes watu hawawezi kujua nini target yako na nini plan yako. Kwahiyo yeyote asiyejua plan yako anaweza akachukulia poa idea yako au kitu ambacho unaenda kukifanya na kukidharau. Lakini siku kitakapoleta matunda, ndio watu husanuka na kuona ‘kumbe hii ndio ilikuwa maana yake.”

“Kwahiyo tungesubiri kwanza tukaona matokeo, tutafeli au tutaweza kufaulu. Watu wakianza kujudge mapema na kukilaani mapema kitu ambacho ni plan nzuri tu za faida na biashara, si poa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents