Habari

Muhimbili kuanza kutibu magonjwa kama India mwaka 2017

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imeanza kutekeleza azma ya serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje kwa vitendo ambao walikuwa wakifuata matibabu yasiyopatikana hapa nchini.

muhimbili

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha Mkatika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya hospitali kwa kipindi cha mwaka mmoja wa awamu ya tano ya utawala wa Rais Dkt John Joseph Magufuli.

“Katika kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano, utawala wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Joseph Magufuli tumefanikiwa kupunguza wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje na kufanikiwa kuokoa gharama zaidi ya asilimia 50 kwa mwaka,” alisema Aligaesha.

“Wajibu wetu hasa ndio huu na sasa tumeanza kushika nafasi yetu kama hospitali ya taifa Muhimbili na kusimama pale. Kwa kuanza tunatekeleza agizo hili au azma hii kwa vitendo, tunatarajia ifikapo January 2017 kuanza huduma ya upandikizaji wa figo hapa Muhimbili. Jitihada tumeshaweka tumepeleka wataalamu karibu 20 India kujifunza upandikizaji wa figo kwa wagonjwa na tunawatarajia kurejea nchini mwishoni mwaka huu. Jitihada ya maeneo ya kufanyia huduma tumekwisha anza kama vyumba vya upasuaji na ICU vyote vimekwisha anza maandalizi tunatarajia ifikapo mwishoni mwa mwaka huu maeneo ya kutolea huduma yatakuwa yamekamilika,” aliongeza.

“Lakini mjue kama huduma hii ya kupandikiza figo tutaifanya hapa ambayo huwa ukipeleka mgonjwa nje inagharimu milioni 40 mpaka 60 maana yake ni kwamba mgonjwa akifanyiwa hapa hapa nchini gharama itapungua karibu nusu ya gharama inaweza ikashuka karibu asilimia 40 mpaka 50 kwahiyo kama mgonjwa mmoja ametumia kiasi kile cha fedha basi fedha ile wanaweza wakatumia watu wawili,watatu, mpaka wanne”,alieleza.

Aliendelea kufafanua, “Hospitali tulituma wataalam saba nchini India katika hospitali za Apollo ambazo ni bingwa pia na zina uzoefu mkubwa katika mambo hayo ili wakajifunze kwa njia ya vitendo jinsi ya kufanya upasuaji na upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto ili kuweza kuokoa shilingi na wamesharudi nchini wiki iliyopita kwaajili ya kuendelea kufanya kazi.”

“Wakati wowote Disemba tutaweza kufanya huduma ya hiki kifaa cha kupandikiza kifaa cha usikivu hapa hapa Muhimbili mgonjwa mmoja akipelekwa nje kwaajili ya kupandikizwa kifaa cha usikivu inaigharimu serikali kiasi cha shilingi milioni 70 mpaka 100 tukifanya hapa hiyo gharama itapungua asilimia 50 mpaka 40 maana yake wigo wa watu kuhumia unaonekana.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents