Michezo

Frank de Boer atimuliwa Inter Milan baada ya kudumu kwa siku 85

Hatimaye kocha Frank de Boer amefutwa kazi na klabu ya Inter Milan ya Italia baada ya kufanya kazi kwa siku 85 pekee ambapo amepoteza mechi nne ligini.

_92204144_epadeboer

Inter wapo nafasi ya 12 kwa sasa Serie A baada ya kushindwa 1-0 Sampdoria Jumapili.

Hiyo ilikuwa mechi yao ya nne kushindwa katika mechi tano za ligi walizocheza chini yake msimu huu.

De Boer, 46, alikuwa beki wa Uholanzi enzi za uchezaji wake na aliwahi kuwa mkufunzi wa Ajax.

Alihusishwa na kuhamia klabu za Everton na Southampton majira ya joto.

Inter watakutana na Southampton ligi ndogo ya Ulaya, Europa League siku ya Alhamisi.

Mkufunzi wa timu ya vijana Stefano Vecchi atakuwa kwenye usukani mechi hiyo.

Wakati wa uchezaji wake, alichezea Ajax, Barcelona, Galatasaray na Rangers.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents