Burudani

Muigizaji wa Home Alone afariki dunia

Aliyekuwa muigizaji wa Home Alone1,Home Alone 2 na Lost in New York, John Heard ameripotiwa kufariki dunia akiwa katika chumba cha hoteli moja jijini Callifonia.

Muigizaji huyo ambaye amepata umaarufu kupitia filamu hizo zilizotamba miaka ya 90, amefariki akiwa na miaka 72, Mpaka sasa chanzo cha kifo cha muigizaji huyo hakijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, marehemeu alikuwa amejipumzisha katika hoteli hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji siku ya Jumatano katika kituo cha afya cha Stanford. Marehemu ameacha mke Margot Kidder na mtoto wake mmoja aitwaye John Matthew “Jack”.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents