Habari

Kuongoza nchi lazima uwe mkali – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli ameagiza watu waliojenga kwenye hifadhi ya barabara na reli, nyumba zao zibomolewe huku akisisitiza kuwa muda mwingine kuongoza nchi ni lazima uwe mkali kidogo.

Tokeo la picha la rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli

Rais Magufuli amesema katika utawala ni mateso kwa mawaziri ambao wapo chini yake kwa sababu inawabidi mawaziri hao muda mwingine kushiriki mateso ambayo yeye anayapata hasa linapokuja suala la kuhakikisha wananchi wanapata maisha bora.

Nasikia kuna baadhi ya watu, tena wanaCCM wanawaambia eti msibomoe, mimi naagiza bomoeni zote na tena anzeni na nyumba za wanaCCM”,amesema Rais Magufuli jana mkoani Tabora wakati akizindua barabara ya kutoka Kaliua hadi  Kazilambwa iliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 61.

Hata hivyo mbali ya uzinduaji wa barabara hiyo, Rais Magufuli amempa mwezi mmoja Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuhakikisha kuwa barabara inayounganisha Kaliua na Urambo yenye urefu wa kilometa 28 inajengwa kwa kiwango cha lami.

Saa zingine kuongoza nchi lazima uwe mkali, hata kwenye familia yako usipokuwa mkali watakuchezea mno…Ninawaamini ndiyo maana natoa maagizo haya hadharani, nisingewaamini nisingeagiza, mnafanya kazi nzuri”,amesema Rais Magufuli .

Kwa upate mwingine, Rais Magufuli amesema wananchi wa Tabora wameteseka kwa muda mrefu kwa kukosa barabara bora, hivyo chini ya Serikali yake ni lazima barabara zote zijengwe kwa kiwango cha lami na kwa ubora unaotakiwa.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents