Michezo

Sanchez hajaomba kuondoka  Arsenal – Wenger

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema Paris Saint-Germain inahitaji kumsajili mchezaji wa Barcelona, Neymar kwa sababu wanafahamu kuwa hawawezi kumpata Alexis Sanchez.

Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez

Bosi huyo wa Gunners amesisitiza kwamba mchezaji wake Sanchez hajaomba kuondoka katika klabu hiyo hasa katika usajili wa majira haya ya joto.

Wenger ameendelea na msimamo wake wa kumshikilia Sanchez kwaajili ya mipango yake ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Wenger amesema kuwa “Hajaomba kuondoka, PSG haiwezi kumsajili Sanchez ndiyo maana wameelekeza nguvu zao nyingi kwa Neymar.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger

“Tupo katika nafasi nzuri kifedha, Sanchez amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake wa kuihudumia Arseanal na hatuna haja ya kutengeneza  fedha zaidi.

“Atakuwa sehemu ya timu yetu hapo mwakani na baada ya hapo tutafahamu kitakachoendelea.

“Kama una mchezaji mzuri huwezi kuzuia kujitokeza kwa timu nyingine kumuhitaji, niswala ambalo linaumiza lakini nilazima upambane nalo”,amesema Mfaransa huyo akiwa katika ziara ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu nchini Uingereza huko Beijing.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents