Soka saa 24!

Mwanamke mmoja ahukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kumkumbatia msanii wa kiume jukwaani (+Video)

Mwanamke mmoja ahukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kumkumbatia msanii wa kiume jukwaani (+Video)

Mwanamke mmoja nchini Saudi Arabia amejikuta akikamatwa na maafisa usalama baada ya kupanda jukwaani na kwenda kumkumbatia mwanamuziki wa kiume anayejulikana kwa jina la Majid al-Mohandis.

 

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Saudi Arabia vimeripoti kuwa mwanadada huyo alipanda jukwaani na kumkumbatia Majid al-Mohandis Ijumaa usiku wakati msanii huyo akitumbuiza katika mji wa Ta’if uliyopo Magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa sheria za Saudi Arabia wanawake hawaruhusiwi kujichanya na jinsia ya kiume endapo hana nasaba naye hivyo mwanamke huyo ameripotiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na faini ya fedha za nchi hiyo ‘riyals’ 100,000 ambayo ni sawa na Tsh 60, 578,491.

Kipande cha video kinachomuonyesha dada huyo akipanda jukwaani na kumkumbatia mwanamziki huyo, Majid al-Mohandis mwenye uraia wa nchi mbili Iraqi na Saudia kimeenea zaidi kwenye mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW