Habari

Breaking News: Mwanasiasa mkongwe ambaye pia aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam ‘Kitwana Kondo’ afariki dunia

Meya wa zamani wa Jiji la Dar es salaam, Mzee Kitwana Kondo amefariki muda mchache uliopita huko katika Hospitali ya Hindu Mandal, ni baada ya kuuugua kwa muda mrefu.

Akithibitisha taarifa hizo Kupitia ITV, mtoto wa Marehemu Stella Kitwana Kondo, anesena Mzee Kitwana Kondo, amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam na mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa kesho 25/5/2017 .

Wakati wa uhai wake Marehemu Kitwana Kondo aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Meya wa manispaa ya Kinondoni.

Marehemu ameacha mjane na watoto watano .

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents