Habari

Mwili wa mtoto waokotwa mtaroni

Mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya mwaka mmoja na miwili umeokutwa ukielea katika mtaro wa maji machafu.

Na Kiyao Hoza

 
Mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya mwaka mmoja na miwili umeokutwa ukielea katika mtaro wa maji machafu.

 

Kamanda wa mkoa wa polisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi amesema tukio hilo limetokea Temeke Mikoroshini, jana saa 9.00 alasiri.

 

Akasema jitihada za kumtafuta mtuhumiwa bado zinaendelea.
Wakati huo huo, Msimazi wa walinzi katika kampuni ya Group Four Security, Twalib Kambangwa,56, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari.

 

Akasema mlinzi huyo alikutwa na mauti hayo alipokuwa amesimama katika makutano ya barabara za Mandela na Kilwa akisubiri kuvuka.

 

Kamanda Kandihabi akasema tukio hilo, ajali hiyo ilitokea jana saa 6.30 mchana.

 

Akasema gari aina ya Layland lenye namba za usajili T 375 ACJ linalotumika kubeba maji machafu, lilimgonga mlinzi huyo.

 

Akasema dereva ambaye alitimka baada ya ajali hiyo, bado hajafahamika na polisi wanaendelea kumsaka.

 

Na mwanamke mmoja , Alhonsina Sangula,31, amefariki dunia baada ya kuangukiwa na tawi la mbuyu.

 

Kamanda wa mkoa wa polisi wa Kinondoni, Jamal Rwambow, amesema marehemu alidondokewa na tawi hilo Jumatatu asubuhi saa 2.00.

 

Akasema baada a kudondokewa na tawi hilo, alipelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu lakini jana alifariki dunia saa 9.00.

 

Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents