Mwizi wa kazi za wasanii akamatwa

COSOTAChama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kikishirikiana na jeshi la polisi hivi kaibuni wamemkamata mtuhumiwa mmoja aliykeuwa akijishughulisha na kutengeneza mikanda na CD bandia zenye kazi za wasanii wa muziki hapa nchini

COSOTA


 


Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kikishirikiana na jeshi la polisi hivi kaibuni wamemkamata mtuhumiwa mmoja aliykeuwa akijishughulisha na kutengeneza mikanda na CD bandia zenye kazi za wasanii wa muziki hapa nchini.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota Yustus Mkinga, mtuhumiwa huyo amekamatwa na vifaa vya kutengenezea mikanda na kwamba kazi alizokuwa anadurufu ni jumla ya kazi 90 za wasanii.



Miongoni mwa kazi ambazo zilifumwa zikiwa zimetengenezwa na mtuhumiwa huyo ni pamoja na ya Upendo Nkone, Sikitiko langu, Mizengwe, Lady JD- Moto, Double Extra, Paka Mapepe, Ng?ang?ania, na Msondo.



Nyimbo nyingine ni pamoja na Mapenzi Kizunguzungu, Yebo Yebo, Haleluya Collection, Mtu Pesa, Dar to Lagos, Utalijua jiji na Akudo Impact.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa vifaa ambavyo alikuwa akivitumia kufyatulia kazi hizo pamoja na masters za kazi vipo mikononi mwa polisi.



Mkinga amewataka pia wale wote wenye hakimiliki au hakishiriki ya kazi hizo kuwasilisha mikataba na nyaraka nyingine zinazohusu umiliki wa kazi zilizotajwa kabla ya April 12 mwaka huu.



Na hata hivyo mtuhumiwa huyo jina lake halikuweza kupatikana haraka.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents