Michezo

Nafasi ya Liverpool ni ipi katika mbio za Ubingwa msimu huu baada ya sare ya pili mfululizo ?

Katika mchezo wa jana ambao uliwakutanisha Majogoo Liverpool dhidi ya wagonga nyundo wa London West Ham United, unaifanya Liverpool kupoteza alama muhimu mbili na ikiwa ni mchezo wao wa pili mfululizo hii ni baada ya sare ya mchezo uliopiya dhidi ya Leicester.

Matokeo haya yanaiopa nafasi kubwa sana Manchester City licha ya upishano wa alama 3 tu kwenye msimamo ingawa zoote zimecheza michezo sawa,

Ikumbukwe Ligi bado haijaisha, kuna mechi 13 zilizosalia kuchezwa, laikini kwa mashabiki wa Liverpool tayari kuna hofu inayoanza kujengeka. Sare mbili mfululizo ambazo Liverpool wamezipata katika mechi zao za Ligi ya Premia hivi karibuni zinazidi kufanya mpambano wa kunyakuwa ubingwa kuwa mgumu zaidi.

Hali hiyo inaanza kukumbushia machungu ya mashabiki wa Liverpool kwa misimu ya 2008-09 na 2013-14 ambapo timu yao ilipokwa tonge mdomoni katika dakika za mwisho.

Liverpool, maarufu kama majogoo wa jiji hawajanyanyua ubingwa wa Ligi ya England toka mwaka 1990.

Mara mbili katika wiki nne zilizopita Liverpool ilikuwa na nafasi ya kutanua pengo la uongozi kileleni mwa Ligi ya Premia kwa alama kubwa hali ambayo ingewafanya wawe na nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa.

Nafsi ya kwanza ilikuwa pale walipokutana na Manchester City Januari 3 ambapo kulikuwa na uwezekano wa kutanua pengo kwa alama 10. Kabla ya Mechi hiyo Liverpool walikuwa wakiongoza kwa alama saba dhidi ya City.

Liverpool hata hivyo walipoteza mchezo huo kwa goli 2-1 na kufanya pengo lipunguwe na kufikia alama nne.

Januari 29, City walifungwa na Newcaste goli 2-1. Liveroop walikuwa na wasaa wa kutanua pengo kwa alama 7 laiti wangeliwafunga Leicester City siku moja mbele. Hata hivyo Liverpool ilitoka sare ya 1-1 katika mchezo huo uliopigwa Januari 30, na kufanya pengo liwe alama tano.

Klopp alilama kuwa theluji iliyokuwa imedondoka uwanjani iliwazuia kupata matokeo bora uwanjani.

Jana Liverpool ilirejea tena dimbani dhidi ya West Ham ambapo walitoka sare ya 1-1 tena. Wikendi, City waliwabamiza Arsenal goli 2-1, hivyo kwa matokeo hayo pengo sasa limepunguwa mpaka alama tatu baina yao.

Hili ni anguko kubwa kwa Liverpool na habari njema kwa Man City. Tofauti kati yao ilikuwa alama tisa Disemba 29.

Endapo Man City itashinda mchezo wake dhidi ya Everton kesho Jumatano wataongoza msimamo wa Ligi ya Premia kwa tofauti ya magoli.

Tottenham pia bado wangali katika mbio za kusaka ubingwa wakiwa na alama 57, alama tano tu nyuma ya Liverpool.

Sergio Aguero wa City ambaye alifunga goli dhidi ya Liverpool mwezi Januari ameendelea kuwa tishio kwa kufunga goli tatu peke yake dhidi ya Arsenal Jumapili.

Historia pia haipo upande wa Liverpool katika mbio za kuwania ubingwa wa EPL.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa timu ambayo inaongoza EPL wakati wa msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya kuchukua ubingwa.

Katika misimu 10 iliyopita ya EPL, ubingwa ulienda kwa klabu iliyokuwa ikiongoza ligi kwenye msimu wa siku kuu hizo mara nane, na katika mara mbili pekee ambazo haikuwa hivyo yaani msimu wa 2008-09 na 2013-14 ni Liverpool ndiyo ilikuwa kwenye usukani.

Swali miongoni mwa wapenzi wa mpira ni kuwa, kwa namna Ligi inavyoendelea, mkosi huo utawakumba tena Liverpool kwa mara ya tatu?

Chanzo: https://www.bbc.com/swahili/michezo-47129749

By Ally Juma.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents