Habari

Nafundisha bure vijana kujitegemea kujiajiri – Eunice Manamba (+Video)

Mama Eunice Manamba ameanzisha ‘program’ itakayoweza kuwasaidia vijana kujitambua na kuweza kujiajiri hali ambayo itaweza kuwasaidia katika kujiongezea kipato badala ya kusubiri kuajiriwa.

Manamba amesema kuwa ameanzisha mafunzo hayo bure kabisa ili kuwasaidia vijana kuweza kutimiza ndoto zao katika kujiajiri badala ya kusubiria ajira na hivyo kujikwamua kiuchumi.

”Itawasaidia vijana waondokane na wazo kwamba nikisha maliza kusoma niende ni kaajiriwe…. nimeona watu wengi wamejiajiri na kuweza kufika mbali. Nitatoa mafunzo bure kila Jumatano na Jumamosi hapa Sinza Madukani.

Akizungumza mbele ya waandishi, Mama Eunice Manamba ameongeza kuwa kupitia simu ya mkononi kama kijana unaweza kubadili maisha yako kwa kuwa mjasiriamali na kuweza kujikwamua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents