Habari

Nairobi yaonja joto la Dj Cleo


Mzee wa Facebook usiku wa kuamkia leo amedondosha bonge la show jijini Nairobi Kenya katika show iliyokuwa imepewa jina la FAHRENHEIT PARTY.

Akiwa na madancer wake The Teddy Bears na Dj Soul T aliwafanya mashabiki wake kuutumia vema usiku wa kuamkia leo kwa show kali iliyokuwa na nyomi la kufa mtu.

“That was a night well spent ‪#FAHRENHEITPARTY‬ – Big up @djcleo1,” aliandika shabiki mmoja.
Ilibidi ajifunze Kiswahili cha kuombea maji ambapo muda mfupi baada ya show alitweet, “ NAIROBI…. nataka msichana mrembo niyende naye south africa Akowaphi????? Hands up.” Japokuwa hatuna uhakika kama maneno haya aliyasema kwenye stage wakati akiendelea na show.

Dj Cleo alisindikizwa na wasanii kutoka Kenya ambao ni pamoja na kundi la Camp Mulla, Just A Band na Madtraxx.
Kuna kitu kimoja tu ambacho Dj Cleo kilimsikitisha jijini Nairobi kama alivyotweet kabla ya show, “FACT: Kenya has a shortage of ice, haven’t been able to get a drink with ice, I hope there’s some tonight when I get on stage LOL.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents