Burudani

Namna utavyoifaidi albamu ya Joh Makini ‘God Engineering’

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Joh Makini amefunguka jinsi mashabiki wake watavyoifurahia albamu yake mpya inayokuja, God Engineering.

Joh Makini ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa katika utoaji wa albamu hiyo kutakuwa na vitu viwili; mosi, albamu yenyewe na The Best of Joh Makini.

“Kuna kitu kimoja nimekisema kwenye huu mfumo wa uuzaji wa albamu, kuna CD itakuwa ya albamu ya Joh Makini inaitwa God Engineering. Halafu kuna The Best of Joh Makini ya ngoma zile ambazo zilitoka lakini bado watu wanakiu ya kuzisikiliza, hizo pia zitakuwa kwenye CD yake,” amesema.

Rapper huyo kutoka kundi la Weusi kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Mipaka’ ambayo leo ameiachia rasmi katika radio station.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents