Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Nandy adai yeye ndiye msanii wa kike namba moja Tanzania, ataja nafasi ya Vanessa na Lady Jaydee

Msanii wa Bongo Flava, Nandy amedai kuwa kwa sasa yeye ndiye msanii wa kike namba moja Tanzania.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Ninogeshe’ ameiambia Break, Clouds TV kuwa yeye ni namba kwa kigezo cha namba ila anawaheshimu wale wote waliomtangulia kimuziki.

“Namba moja kwa Tanzania sasa hivi, au wewe unaonaje?, go with numbers, go YouTube, go Subscriber, go every where, go with numbers. Usiangalie tu nani anafanya nini, angalia numbers,” amesema Nandy.

“Kabla sijawa namba moja, namba moja yangu Lady Jaydee lakini bado nitamuheshimu, ni mkubwa amenitangulia. Yeyote yule ambaye amenitangulia lazima nimuheshimu kwamba ni mkubwa,” amesisitiza.

Nandy ameendelea kwa kusema kuwa ingawa wapo wakubwa kwake na waliomtangulia lakini haimaanishi kuwa watakuwa namba moja siku zote lazima kuna kubadilishana nafasi.

Hata hapo awali alipoulizwa kati ya Vanessa Mdee, Ruby na yeye yupi anastahili kuwa namba moja, bado alisisitiza yeye ni namba moja huku Vanessa Mdee na Ruby wote akiwapa namba mbili.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW