Burudani ya Michezo Live

Napoleon akanusha kumpa Wema nafasi ya upendeleo kuigiza filamu mpya, XBaller

Muigizaji wa filamu ya Going Bongo, Ernest Napoleon, amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja la kila siku kuwa amempa Wema Sepetu nafasi ya upendeleo kuigiza kwenye filamu yake mpya, XBaller.

WEMA2

“Wema ana kipaji. Sio cha kuigiza pekee yake lakini pia “charisma”. Kitu ambacho watu wachache sana duniani wanacho. Ni kipaji cha kupendwa na akiongea lazima umsikilize. Watu kama Hillary Clinton, Will Smith, Kanye West na hata Elizabeth Michael “Lulu” wanacho,’ Napoleon ameiambia Bongo5.

“Lakini ukweli ni kwamba mara ya mwisho kuongea naye ni zaidi ya miezi mitatu na sijaongea na mwandishi yeyote kuhusu Wema kuwepo kwenye filamu hii ya XBaller. Kulikuwa na fikira za kumu-approach wakati nafanya Going Bongo kwenye part ya Nesi Tina lakini ilikuwa ngumu kidogo. Part aliyocheza Mkenya Nyokabi Gethaiga. Hivi sasa tunafanya usaili wa kutafuta vipaji Tanzania. Tumeshafanya usaili wa wasichana Dar. Tunategemea kufanya Arusha, Mwanza na Kati ya Mbeya au Iringa,” ameongeza.

index

“Kuhusu nafasi za “upendeleo”. Kuna msanii mmoja tu ambaye naweza ku-confirm kwamba kwa asilimia 90 atakuwepo kwenye movie hii. Jina lake ni Ann Kansiime ambaye ni mchekeshaji kutoka kwa jirani zetu Uganda. Part ninayotarajia acheze imefanana na personality yake ya uchekeshaji.”

“Lakini jambo hilo litaamuliwa na director wa filamu hii ambaye ni Darius Britt kutoka Marekani na Kansiime mwenyewe. Kwa sasa ni mapema kidogo.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW