Burudani

Navy Kenzo wakiri muziki kuwa na stress, kivipi?

By  | 

Msanii wa muziki Bongo na producer, Nahreel ambaye ni member wa kundi la Navy Kenzo, amesema wasanii wachanga ni vema kusaidiwa kutokana muziki una changamoto sana.

Nahreel amesema hayo wakati msanii wa kutoka Nigeria Patoranking akimtambulisha msanii mpya aliyemsaini katika label yake kutoka Tanzania.

“Unajua muziki una stress nyingi na alipotokea yeye anajua kwa hiyo anajaribu kutumia experience yake kumrahisishia mwingine, huo ni moyo wa kipekee sana,” alisema.

Patoranking kutoka Nigeria amemsaini Walid kupitia label yake inayotokwenda kwa jina la Amari Music. Utakumbuka kuwa kundi la Navy Kenzo limeshafanya kolabo Patoranking inayofahamika kama Bajaj.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments