Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Nazunguka sana kufanya show Congo, Burundi na ninajaza – Hemedy PhD

Msanii wa muziki Bongo na muigizaji wa filamu Bongo, Hemedy PhD amesema muziki wa sasa umetoa nafasi kwa wasanii kuandaa show zao kuliko kutengemea kuandaliwa.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Mkimbie’ ameiambia 5Selekt ya EATV kuwa yeye amelitambua hilo na sasa amekuwa akifanya show zake mikoani na nje ya nchi.

“Mimi ni mtu ambaye nazunguka sana kwenye kufanya show, miezi sita iliyopita yote nilikuwa niko mikoani, Congo, Burundi na ninajaza kwa sababu platform ya muziki ilipofika sasa hivi don’t depend on promoter akupe shows, unaanda mwenyewe na raia wanasikia wanakuja wanaimba ngoma mwanzo mwisho” amesema.

Ameongeza kuwa kitu kingine ambacho sasa hivi kimekuwa advantage kwa wasanii ni kuwa mashabiki hawasubiri ngoma ipingwe kwenye radio au tv  bali kama ni nzuri wanaitafuta katika mtandao kitu ambacho kimekuwa msada mkubwa kwa wasanii wasio na team kubwa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW