Michezo

Nendeni mkawaambie nimerudi – Juma Nyoso

Beki wa klabu ya Kagera Sugar, Juma Nyosso ameibuka na kuweka wazi malengo yake ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara.

Beki wa klabu ya Kagera Sugar, Juma Nyosso

Nyoso ambaye ni miongoni mwa wachezaji wapya sita katika kikosi cha Kagera Suger amerejea kwenye soka baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya miaka miwili iliyotokana na kitendo cha utovu wa nidhamu uwanjani.

Beki huyo maarufu wa zamani wa Simba SC amerejea katika Ligi Kuu Bara kwa lengo lengo lakusaidia timu yake kufanya vizuri.

“Napenda niwaambie watu kwamba nimerejea tena katika soka na nimekuwa mpya tofauti na yule wa awali ambapo sasa nimekuja na nguvu mpya ya kuipambania timu yangu ifanye vizuri.

“Nina uhakika mkubwa wa kutamba kwenye ligi msimu ujao kwa sababu bado nina uwezo kuliko hata mabeki wengi waliokuwa wanacheza ligi, kiufupi wengi watarajie kitu kipya kutoka kwangu,” alisema Nyosso.

Timu ya Kagera Sugar ya Bukoba ipo katika maandalizi  ya kujianda na msimu mpya 2017/2018 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza Agosti 26, mwaka huu.

Kagera mpaka sasa imewasajili wachezaji, Said Kipao, Peter Mwalyanzi, Omary Daga ‘Dagashenko’, Venance Ludovic pamoja na Japhary Kibaya.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents