AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Neville amshauri kocha wa Arsenal Emery kutumia mfumo huu kama anataka matokeo mazuri

Neville amshauri kocha wa Arsenal Emery kutumia mfumo huu kama anataka matokeo mazuri

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United na Everton Phil Neville amemshauri Kocha wa Arsenal Unai Emery kuwa anapaswa kushikilia mfumo mzuri utakaompa matokeo mazuri katika kila mchezo.

Neville ameongea hayo na kusema ” Ukiangalia ushindi wa Arsenal chini ya Unai katika mechi yake ya mwisho ambapo aliwatumia Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang tangu mwanzo, waliweza kupata ushindi”

Baada ya kuwa mbadala (sub) katika michezo mitatu ya kwanza ya Arsenal matokeo hayakuwa mazuri sana, Lacazette alipoanza katika mchezo wa mwisho Arsenal ilipata ushindi wa goli 3-2 huko Cardiff City, huku Aubameyang akienda kushoto. Lacazette akifunga goli moja na kufanikiwa kutengeneza nafasi ya goli.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Everton, anaamini kuwa Unai akiwa na Lacazette na Aubameyang kutokana na kwamba wachezaji hao wanakimbia uwanjani,hasa katika mchezo wa Jumamosi watakapo kwenda Newcastle United itasaidia na kuleta matumaini kwa Emery kupata  ushindi wa tatu mfululizo.

“Watafunga magoli mengi zaidi, wana uelewano mzuri pia wanauharaka ulio bora zaidi,” Neville aliongeza. ” Mabeki wengi hawapendi kucheza dhidi yake [Lacazette] kwa sababu ya Uharaka wake wenye makali, pia ana uwezo wa  kutembea kila mahali akiwa uwanjani.”

“Arsenal ni sehemu bora zaidi kwa upande wao, Wanaonekana vizuri zaidi kwenda mbele”

“Ni tu swali la muda kwa Aubameyang anaweza kujitoa mwenyewe au kuwa na furaha akicheza upande wa kushoto ?.”

Nadharia ya Neville kwamba mashambulizi ya Gunners ni hatari zaidi wakati Lacazette anapoanza inakubaliana na takwimu hizi hapa.

Arsenal wastani wa magoli ni 2.2  mechi wakimwanzisha Lacazette kutoka kick-off, ikilinganishwa na 1.5 wakati hajaanza.angalia takwimu hizi:-

Arsenal in PL 2017/18 to present
Lacazette sakianzaLacazette asipoanza
Played2715
Won165
Drawn51
Lost69
Goals for5923
Goals/match2.21.5
Win %59.333.3
Points/match2.01.1

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW