Ney Mtegoni…

Ney wa Mitego
Baada ya msanii ‘Ney wa Mitego’ kurelease single yake iitwayo ITAFAHAMIKA TU (bofya kuangalia video) ..inayowaponda wasanii wengi waliokuwa maarufu na sasa wamefulia,sasa anapokea simu nyingi za vitisho kutokana na ngoma hiyo.

"Yaani hapa nilipo sipokei simu yoyote nisiyoifahamu kutokana na vitisho ninavyovipata, lakini mimi siogopi chochote kwani ilichokiongea ni ukweli mtupu kwani kwa msanii ambae ataisikiliza vizuri ngoma yangu atanielewa nachomaanisha.

Katika ngoma hiyo Ney kamzungumzia Mr Nice kuwa anauza shanga, Dudu Baya kawa mganga, Sister P anauza pipi, Rah P kawa mhudumu wa guest, Bwana Misosi anafanya kazi hoteli, P Funk ameishiwa na wengine kibao.

Ukiachilia mbali hao baadhi ya tuliowataja jamaa kawataja kibao ndani humo, je mziki wetu unaelekea wapi kwasasa?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents