Habari

Ngoma Africa ndani ya “Afrika Market”

Ngoma Africa BandBendi ya The Ngoma Africa na bongo dansi lake la Tanzania imeteuliwa kutumbuiza katika onyesho kubwa la “Afrika Market” mjini Hamburg nchini Ujerumani.

Bendi ya The Ngoma Africa na bongo dansi lake la Tanzania imeteuliwa kutumbuiza katika onyesho kubwa la “Afrika Market” mjini Hamburg nchini Ujerumani.
waandaaji wa onyesho hilo wameipa bingo bendi hiyo kutokana na utamu wa mziki wa dansi la kitanzania ambalo bendi hiyo ndiyo inayotumia kupeperushia bendera ya Tanzania.
Onyesho hilo litakalo fanyika 2 june 2007 huko Humburg, linatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu,siku hiyo ya ufunguzi wa onyesho hilo kadamnasi ya maelfu ya watu watashuhudia kwa mara nyingine tena! Moto wa mziki mtamu wa dansi halisi la tanzania utakao poromoshwa na vijana wa the ngoma africa,bendi inayoongozwa na mwanamziki,mtunzi na mwimbaji Ebrahim makunja a.k.a ras ebby makunja au Bwana Kichwa Ngumu.Bendi hiyo hita uhakikishia ulimwengu kwa mara nyingine tena kuwa mziki wa tanzania ni moto usiowekeka katika kiganja cha mkono.


Ngoma Africa Band


Source: Ngoma Africa Band

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents