HabariLady Jay Dee

Ngoni Kubanjuka na Lady Jay Dee

Ngoni na Lady Jay DeeWasanii maarufu kuotoka nchini Uganda ‘Ngoni’ wanatarajia kufanya bonge la kolabo na msanii Lady Jay dee, hii imetokana na vijana hao kumkubali ile mbaya mwanadada huyo wa kibongo kutokana na kazi zake anazozifanya

Ngoni na Lady Jay Dee

 

Wasanii maarufu kuotoka nchini Uganda ‘Ngoni’ wanatarajia kufanya bonge la kolabo na msanii Lady Jay dee, hii imetokana na vijana hao kumkubali ile mbaya mwanadada huyo wa kibongo kutokana na kazi zake anazozifanya.

 

“unajua Jay Dee anaweza kuimba tena katika levo ya juu sana yaani ni mmoja kati wasanii wakali East Africa ambao kila kukicha wao hutengeneza hit za kufa mtu that’s Why tumeona si vema kuitumia nafasi hii na kwa ujio huu Tanzania kupiga nae mkono mmoja ambao tuna uhakika utakuwa ni mzuri sana” alisema Patrick Nyanzi a.k.a Patoo wa kundi hilo la ngoni.

 

Vijana hao ambao wanatamba na vibao vyao kama vile ‘mimi na wewe’ waliyoshirikiana na AY, Bigula na nyingine nyingi, wameufurahia sana ujio wao jijini kwani ni siku nyingi sana walikuwana na ndoto za kupita Show Tanzania.

 

Akielezea sababu za wao kuimba ngoma zenye mchanganyiko na lugha ya Kiswahili alisema “unajua kama ni muafrika unapaswa kujifunza lugha karibu zote barani afrika na ukishindwa kuzijua zote basi hata tatu, tunaamini katika list ya lugha za kimataifa Kiswahili nacho kimo, tunajisikia faraja sana kumix na Kiswahili katika ngoma zetu” alisema Eddy Mpangi.

 

Pamoja na yote hayo linasubiriwa hilo dude lao watakalofanya na Lady Jay Dee, ambalo mpaka sasa haijajulikana litarekodiwa katika studio gain na prodyuza gani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents