Nick Canon aiweka jumla kwa Mariah Carey

Walifunga ndoa ya siri mwishoni mwa mwezi uliopita na baada ya hapo walienda kujipumzisha kwenye visiwa vya Bahamas kwa muda wa siku kumi na nne kabla ya kurejea kwenye makazi yao

Nick na Mariah



Walifunga ndoa ya siri mwishoni mwa mwezi uliopita na baada ya hapo walienda kujipumzisha kwenye visiwa vya Bahamas kwa muda wa siku kumi na nne kabla ya kurejea kwenye makazi yao.


 


Kila mmoja aliyesikia habari juu ya mastaa hawa wawili, Mariah Carey, anayetamba kwa kuwa na sauti nzuri na Nick Canon, muigizaji maarufu kuwa ni wanandoa wapya alishangaa sana kwani uhusiano wao ulikuwa wa siri sana na hakuna mtu aliyewahi kustukia hili.


 


Gharama za pete za wanandoa hawa ilizua utata kwa kila mtu kwani pete hizo ziligharimu jumla ya dola za kimarekani milioni 2.5 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 3 za kitanzania


 



“Nataka nifanye kitu kwa Mariah ambacho naamini kabisa atakipenda na kuthamini kwani ni mwanamke maalumu kwa ajili yangu” Canon. Habari kutoka kwa mmoja wa mmiliki wa hilo duka la vito vya thamani la Jacob & Co., ambapo Mariah na mumewe walinunua pete hizo alisema “Nick alikuwa hana la kusema zaidi ya nampenda sana Mariah na anahitaji kitu kizuuri kama alivyo”.


 



Aliendelea kusema “Mariah naye alikuwa makini na uchaguzi wa pete hizo na alichukua pete yenye vito ambavyo ni vya beii ya juu kuliko vyote dukani hapo”. Vilevile wanandoa hao walioruhusu jarida la ‘People’ kuchukua picha zao walikuwa na michoro tofauti migongoni mwao ambapo Maraih alionekana kuwa na mchoro ulioandikwa ‘Mrs Canon’ huku Nick akiwa na mchoro ulioandikwa ‘Mariah’.


 


Nick aliulizwa kuhusiana na michro hiyo na kujibu ‘Hii ina maana sana kwetu,haatukuwahi kufikiria kufanya hivi,tuna furaha,tunapendana na ndiyo maana nimekubali kujichora jina lake na vilevile yeye kuwa na jina langu mgongoni kwake”.



 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents