AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Nicki Minaj aweka wazi ujio wa albamu yake mpya

Baada ya kimya cha takribani miaka minne bila ya albamu sokoni, Nicki Minaj anarudi tena kwa kishindo kikubwa.

Malkia huyo wa muziki wa Hip Hop ameweka wazi kuwa albamu hiyo itatoka Juni mwaka huu na itaitwa ‘Queen’.

Nicki amesema hayo Jumatatu hii kwenye red carpet ya onyesho la mitindo na mavazi Met Gala lililofanyika mjini New York huku akiwa amevalia gauni la rangi nyekundu lililobuniwa na Oscar de la Renta aliyefariki Oktoba 2014.

“Ni usiku mkubwa kwangu kwa sababu ninataka ulimwengu ufahamu kuwa albamu yangu inakuja Juni 15, na inaitwa ‘Queen’, siwezi kusubiri,” amesema mrembo huyo.

Albamu ya mwisho ya Nicki Minaj ilikuwa inaitwa The Pinkprint (2014) ambayo ilifanikiwa kutinga namba moja kwenye chati za Billboard 200.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW