Tupo Nawe

Nigeria kuanza kutengeneza magari ya umeme mwakani, ‘Tunataka nchi yetu iwe kama China’

Ikiwa ni miaka 59 imepita tangu taifa la Nigeria lipate uhuru, Hatimaye taifa hilo kuanzia mwakani 2020 litaanza kuunda magari yanayotumia umeme jua.

Akiongea kwenye maonesho ya teknolojia ya umeme jua Jana Oktoba 2, 2019 mjini Ibadan, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya umeme jua ya (SECODI), Moses Onaja  amesema kuwa magari hayo yatasaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na gharama za maisha.

Tunataka tuishawishi jamii ianze kutumia nisharti mbadala ili kunusuru mazingira yetu, Mungu akipenda kampuni yetu kuanzia mwakani tutaanza kuunda magari hapa Nigeria yatakayotumia umeme jua. Kila kitu kipo tayari tutaanza na magari madogo 20,000 ambayo yatauzwa kwa bei rafiki kwa Wanaijeria,”

Tunachokihitaji kwa sasa ni ushirikiano tu kutoka Serikalini, Tunataka kila kitu kifanyike hapa Nigeria iwe kama China wanavyofanya,” ameeleza Onaja.

Onaja amesema kuwa Kampuni yake imefanya utafiti kwa miaka 6, Na hadi kufikia mwaka huu tayari imefanikiwa kuunda gari kadhaa za umeme jua kama za majaribio.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW