Nikiandika wimbo na kalamu nyekundu unakuwa hit balaa – Chidi Benz

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Chid Benz amedai katika maisha yake ya kimuziki ikitokea akaandika wimbo na kalamu nyekundu ni lazima ifanye vizuri (hit).

Rapper huyo ameiambia Clouds Fm kuwa kitu hicho kilitokea katika kolabo kati yake na Mwasiti ‘Hao’ na alimueleza wazi muimbaji huyo kuwa hiyo ngoma ingekuwa kubwa kabla hata ya kutoka.

“Nilimwambia Mwasiti mimi nina tatizo moja nikiandika wimbo na kalamu nyekundu, hiyo ni balaa, hit balaa, lakini sio wewe umeenda kuninunulia dukani unipe,” amesema Chidi Benz.

Katika hatua nyingine Chidi Benz amesema kolabo yake bora kwa muda wote ni hiyo aliyofanya na Mwasiti kwani ilichukua hadi tuzo nchini Kenya.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW