Burudani

Nikusaidieje juuuu Kisima Awards

By  | 

Professor JayMsanii Prof Jay ambaye hivi juzi juzi tu alikamata award za Kilimanjaro kutokana na songi lake ‘Nikusaidieje’..mwishoni mwa wiki ameweza kukaa tena kwenye matawi ya juuu kabisa baada ya kutia kwapani award nyingine

Professor JayMsanii Prof Jay ambaye hivi juzi juzi tu alikamata award za Kilimanjaro kutokana na songi lake ‘Nikusaidieje’..mwishoni mwa wiki ameweza kukaa tena kwenye matawi ya juuu kabisa baada ya kutia kwapani award nyingine ya video bora ya Afrika Mashariki kwa kupitia songi hilohilo kwenye award za ‘KISIMA’ zinazotolewa nchini Kenya.

Tuzo hizo hata hivyo hazikuweza kuhudhuriwa na wasanii kutoka Bongo..kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wa waandaaji,hata hivyo chanzo chetu cha habari kiliweza kuongea na Prof.Jay na kusema kuwa …alipigiwa simu na waandaji kumtaarifa kuwa ameshinda na kwamba wanafanya jitihada za kumtumia tuzo yake…na pia waandaji hao walimwomba radhi kwa kumcheleweshea tiketi ya ndege kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo.

Aidha, Prof akamtaja msanii mwingine wa Bongo aliyefanikiwa kutwaa tuzo ya wimbo bora kuwa ni Langa wa kundi la Wakili kupitia single yake ya ‘Matawi ya Juu’.

”Tunaweza kuwa wengi zaidi lakini hao ndio niliotajiwa katika simu… angalau
tunajenga heshima ya bongo fleva nje ya rnipaka,” akasema.

Msanii huyo aliwahi kukaririwa ktk siku za karibuni akijitamba kuwa kutokana na ubora wa songi lake ‘Nikusaidieje’ ,anastahili tuzo zaidi ya tisa.
Source: Darhotwire

{mos_sb_discuss:6}

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments