Burudani

Ningependa kufanya kazi na Mwana FA tena – Maua Sama

Maua Sama amedai kuwa angependa kufanya kazi tena na bosi wake wa zamani, Mwana FA.

13422923_1651268808529103_1695451904_n

Muimbaji huyo alianza kujulikana kupitia wimbo ‘So Crazy’ aliomshirikisha rapper huyo. Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Maua alisema kuwa FA ni rapper anayemkubali zaidi.

Amewataja Fid Q, Bill Nass, Mr Blue, Weusi kuwa ni rappers wengine ambao angependa kufanya nao kazi na kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa hip hop ya Tanzania.

Aliongeza kuwa ngoma yake ijayo amemshirikisha rapper Stamina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents