Habari

Nizar aitwa Tottenham

Nizar aitwa Tottenham
Kiungo mahiri wa ‘Taifa Stars’ Nizar Khalfan ameitwa na timu ya Ligi
Kuu ya England, Tottenham Hotspurs kwa ajili ya kufanya majaribio ya
kucheza soka ya kulipwa

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa na Mkurugenzi Mkuu wa Moro United, Azim Dewji  ilieleza kuwa Nizar mwenye umri wa miaka 21 anatarajia kuondoka mwishoni wa mwezi huu kwa majaribio yatakayoanza Juni mosi chini ya kocha Harry Redknapp.

Taarifa ilieleza kuwa moja ya mikakati ya Moro United ni kusajili wachezaji wengi wenye umri mdogo, ili wakulie mikononi mwao wakiamini wataweza kufundishika na kuwa rahisi kuwapeleka katika klabu za Ulaya na kwingineko.

Tottenham ni moja ya timu maarufu zinazocheza Ligi Kuu England na imewahi kutamba na nyota kadhaa kama Gary Lineker, Teddy Sheringham, Paul Gascoigne `Gaza’, Jurgen Klinsmann, Sol Campbell na Dimirtar Berbatov.

Kwa upande mwingine Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbrazil Marcio Maximo amesifu utaratibu wa wachezaji wa Stars kupata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi hasa Ulaya kwamba unasaidia kuwajenga wachezaji hao.

Kocha huyo alikuwa akizungumzia umuhimu wa wachezaji wa Stars kupata nafasi za kwenda Ulaya na kuwa muda wa majaribio wanaopata katika klabu hizo huwasaidia kujijenga kimbinu na kisaikolojia, hivyo kurahisisha kazi ya kocha na benchi la ufundi wanaporudi kwenye timu ya taifa.

“Ni jambo zuri kwa wachezaji wa Stars kupata nafasi kama hizo na ningependa hata timu nzima ipate nafasi hiyo ya kufanya majaribio na wafanikiwe katika majaribio yao kutokana na umuhimu wa kuwa na wachezaji wa kulipwa katika timu kama Stars, ”alisema Maximo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents