Michezo

Nwankwo Kanu kuzindua hospitali yake ya moyo yenye gharama ya zaidi ya Tshs bilioni 50

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya soka la Nigeria, Super Eagles Nwankwo Kanu, anatarajia kuzindua hospitali yake ya magonjwa ya moyo March 14 iitwayo Kanu Cardiac Hospital jijini Abuja.
kanu-595x270
Hospitali hiyo yenye thamani ya naira bilioni 5 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 50 za kitanzania itakuwa ikihusika na magonjwa ya moyo kwa watoto. Uzinduzi wa hospitali hiyo utahudhuriwa pia na rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan.

Watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 12 watakuwa wakitibiwa bure kwenye hospitali hiyo. Kanu aliwahi kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo kabla ya kujiunga na klabu Arsenal miaka kadhaa iliyopita. Taasisi yake ya Kanu Heart Foundation imeshawapeleka baadhi ya watoto wenye tatizo hilo kutibiwa nje za nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents