Burudani

Nyimbo za mapenzi nimewaachia Diamond na Alikiba – Mr Blue

Mr Blue amedai kuwa amepunguza kuimba nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi na kwamba amewaachia Alikiba na Diamond wafanye hivyo.

Mr Blue akiimba mashabiki

Akiongea na kituo cha redio cha Kings FM cha Njombe, Blue alisema pamoja na ukweli kwamba wanawake ni mashabiki wakubwa wa nyimbo za mapenzi, amesema nyimbo zake za sasa zinawahusu wanaume watafutaji zaidi.

“Hatuwezi wote tukafanya kitu kimoja kwasababu kuna wanaume pia kwa mfano hawa teenagers ambao ndio wameamka kwenye maisha, watu wamekata tamaa, wana ndoto za kufika mbali so wengine hawafikirii tu mapenzi,” alisema.

“Kwahiyo mimi nikaona mambo hayo ya wanawake sio mbaya kama nikiwaachia akina Alikiba, Diamond na mimi nikadeal na vijana,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents