Burudani

Soggy Doggy asema ili msanii mkongwe asipotee, aepuke kushindana na wasanii wapya

Rapper na mtangazaji wa redio, Soggy Doggy amesema kama msanii mkongwe hataki kupotea kwenye muziki, aepuke kushindana na wasanii waliopo.

11098248_339260619598003_745814393_n

Soggy ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa anarejea kwenye muziki bila kushindana na mtu yoyote hali ambayo amedai itampa nafasi ya kufanya vizuri.

“Kwenye muziki huu sioni kitu kipya sio kwamba nachukia muziki unavyoenda lakini sioni kitu kipya kwenye game, bado naiona nafasi ya wakongwe,” amesema. “Bado naona nafasi yangu, mimi nafasi yangu ipo. Na ukihitaji nafasi yako isiwepo, fanya mashindano na waliopo sasa hivi. Mimi sishindani na mtu yoyote kwenye muziki huu.”

“Kwahiyo mimi sitaimba nyimbo za kinageria kwa sababu mimi sio mnigeria, ni mtanzania. Mimi sitaimba nyimbo za ki-south Africa kwa sababu mimi sio m-south Africa, ni mtanzania. Kwa maana hiyo nitakomaa na aina yangu ya muziki. Hata hii ngoma yangu ‘Nafunga Zipu’ ni aina ya muziki wa Soggy sio muziki wa Jay Mo wala Professor, wala Diamond wala Alikiba. Ni aina ya beat zangu, ni aina ya utunzi wangu ni aina ya idea zangu. Kwa maana hiyo natambua kabisa kuna wengi wana mix idea za aina hiyo na muziki wa aina hiyo.

Narudia tena aina ya muziki wangu sio aina ya muziki wa primary, ni watu walioajiriwa na watu walio maofisini au watu wazima. Watu ambao wanapambana na maisha, watu wenye familia zao, kwa maana hiyo nimeamua kuweka akili yangu kwa hao watu,” amesisitiza Soggy.

Katika hatua nyingine Soggy amesema kwa sasa ataanza tena kufanya kazi mfululizo.

“Sasa hivi sitafanya muziki kama leisure,” anasema Soggy. “Sitafanya muziki kama kitu cha nje, nitaendelea kufanya muziki kama my first love au kitu ninachokipenda zaidi. Kwahiyo wategemee baada ya hii ngoma nitafanya video yake, video ambayo nina imani itakuwa ni nzuri sana. Lakini baada ya hiyo video sio nitakaa sana kawa awali, sasa hivi itakuwa ni kitu baada ya kitu. Ngoma ninazo nyingi sio wakati nipo kimya nilikuwa sirekodi, nilikuwa narekodi kazi. Kwahiyo watu wapokee ngoma yangu mpya production ya Mr T Touch.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents