Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Nyota za Fid Q kwa Khaligraph Jones

Msanii wa hip hop Bongo, Fid Q amesema rapper kutoka Kenya, Khaligraph Jones anapotoa ngoma huitafuta na kuisikiliza kitu ambacho si kawaida kwake.

Kauli ya Fid Q inakuja mara baada ya Khaligraph Jones kueleza kuwa Fid Q ni miongoni mwa wasanii anaowakubali kwa sana kutoka Afrika Mashariki.

“Mimi binafsi naamini Khaligraph Jones yupo katika familia, kwa hiyo kama ambavyo amekuwa akifurahia kupenda kazi zangu na mimi pia huwa nafurahia kazi zake,” amesema.

“Khaligraph ni miongoni mwa wasanii ambao wakitoa ngoma huwa natafuta na kusikiliza, kitu ambacho sio cha kawaida kwangu,” Fid Q ameiambia Wasafi TV.

Khaligraph Jones ambaye hapo juzi ameachia albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Testimony1990, ameshafanya kolabo na rapper kadhaa kutoka Bongo kama Rosa Ree, Young Killer na Nikki Mbishi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW