Habari

Nywele Fupi ama Ndefu?

Flaviana Matata alipopata Umiss Universe Tanzania mnamo 2007, yeye aliwakilisha kila kitu kilichoeleza na kinachoeleza uzuri  wa Kiafrika. Kilichomfanya ajitokeze kwa aina yake ni kichwa kilichonyolewa vizuri miongoni mwa nywele ndefu za washindani wengine. Alijichukua kwa kujiamini na kwa utanashati, mara kwa ghafla wanawake wakaonekana wakielekea salun au kwa kinyozi kunyolewa upara!

Sasa mnamo 2010, mtindo wa nywele ndefu umerudi na wanawake wanawekeza muda wao mwingi katika ususi, mawigi au vibandiko na rasta, na chochote kingine kinachoenda na mtindo huo, ambapo nywele fupi na vipara vimewekwa vimeondolewa kutoka ulingo wa mitindo.

Hata hivyo, umwonapo mwanamama Mwafrika mwenye kichwa kilichonyolewa upara, masikioni amevaa ushanga, na kuvalia nguo ya mtindo wa kisasa, inabidi ufurahie ujasiri wake wa kuendelea kuwa na mwonekano wa mtindo uliopita hali anaendelea kuonekana mzuri.

Uzuri wa mwanamke unahusiana na utamaduni anamoishi. Pale ambapo utamaduni mmoja unaona kuwa kitu fulani ni kizuri, utamaduni mwingine unaona vinginevyo. Katika baadhi ya tamaduni za Kiafrika na Kiasia, wanawake huvaa pete za shingoni kurefusha shingo.

Katika utamaduni wao hiyo shingo ndefu ni dalili ya uzuri, ijapokuwa tamaduni nyingine zinaliona jambo hilo kuwa  la ajabu na la kudhalilisha, wengine wanaweza kudiriki kusema ni mateso ya aina fulani.

Huko China mnamo karne ya 10, wachina walizoe kufunga vikanyagio. Waliloweka bandeji katika damu na miti shamba kwa mantiki ya kuzitayarisha. Msichana alipofika umri wa kuanzia miaka 3 hadi 11 mguu mmoja mmoja hulowekwa katika dawa, kucha zikakatwa na miguu kuchuliwa kwa miti shamba. Mambo haya yalifanyika kama matayarisho dhidi ya maumivu makubwa ambayo yangefuata. Kwa mantiki ya kuvifanya vikanyagio view vidogo, vidole vya miguu vilikunjwa kuelekea chini na kubonyezwa kwa nguvu hadi kuvunjika.

Maumivu yalikuwa makubwa sana hata huwezi kuamini! Ndipo ufungaji bendeji ulipoanza ambao ulifanyika kwa kutumia vipande virefu vya kitambaa cha pamba na kukizungushia juu ya kila mguu ili vidole visikunjuke!

Hata hizi desturi za kuvuta nyusi, kutumia uzi kutoa malaika, au kutoa nywele kwa nta, yote haya huumiza, lakini maumivu ni nini kama siyo uzuri… sawa?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents