Obama Aunganisha Watanzania,Kenya.

WATANZANIA wanaoishi mpakani na Kenya katika eneo Isebania, Sirari na Shirati mkoani Mara baadhi yao jana waliamua kukodi magari ya kuwapeleka katika Kijiji cha Kogero Kisumu kuungana na bibi yake Ris Mteule wa Marekani, Barak Obama anayeitwa Sarah Onyango kusherehekea ushindi wake.

WATANZANIA wanaoishi mpakani na Kenya katika eneo Isebania, Sirari na Shirati mkoani Mara baadhi yao jana waliamua kukodi magari ya kuwapeleka katika Kijiji cha Kogero Kisumu kuungana na bibi yake Ris Mteule wa Marekani, Barak Obama anayeitwa Sarah Onyango kusherehekea ushindi wake.

Tangu asubuhi baada ya kupatikana taarifa za ushindi wa Obama mji wa Sirari na Shirati ililipuka shangwe wakishangilia ushindi huo na wengine wakaamua kuingia nchini Kenya bila ya pasi za kusafiria kuungana na familia ya bibi yake Obama ambako kulikuwa kumeaandaliwa sherehe kubwa.

Kilichowavuta wananchi hao kuamua kwenda Kisumu ni mwingiliano wa kidugu ulipo kati ya wakazi wa Shirati na Sirari kwa upande wa Tanzania na wenzao wa Kisumu nchini Kenya kutokana na wengi wao ni wajaluo kabila la bibi yake Obama, Sara.

Habari zilizopatikana kutoka katika eneo la mpaka huo, watu walioamua kwenda Kisumu walikodisha malori kuwapeleka huku wengine wakiachwa wakiendelea kusherehekea kwa kunywa na kucheza muziki ya kijaluo iliyokuwa ikisikika kila mahali.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika miji hiyo kabla ya kuondoka kwenda Kisumu baadhi ya wakazi hao, walisema wamefurahia ushindi wa Obama kwa kuwa sera za chama chake zinawalenga watu wa kipato cha chini na kwamba yeye atadumisha mahusiano mema na nchi zote duniani bila kubagua dini zao.

Nyamhanga Mwita alisema kuwa viongozi wa afrika wajifunze kutokana na uchaguzi wa Marekani kwamba ubabe wa kivita kwa nchi zingine umepitwa na wakati na na kwamba kung’ang’ania madaraka.

Alisema viongozi wajifunze kiongozi anaposhindwa akubali matokeo kama alivyofanya mpinzania wa Obama , John MaCcan wa Republican.

Wakati umati huo ukienda Kisumu kusherehekea ushindi wa Obama kalenda za Marehemu Chacha Wangwe aliyekuwa Mbunge wa Tarime na za Obama zimekuwa zikiuzwa kama njugu katika wilaya za Tarime, Serengeti, Musoma na Bunda.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents