Obama Kidume

Kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kugombea uraisi nchini Marekani kati ya Bi Hillary Clinton na Barak Obama, hivi sasa zinaelekea ukingoni huku Bwana Obama akiwa na nafasi kubwa ya kushinda…

obama_1.jpg

 

Kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kugombea uraisi nchini Marekani kati ya Bi Hillary Clinton na Barak Obama, hivi sasa zinaelekea ukingoni huku Bwana Obama akiwa na nafasi kubwa ya kushinda, baada ya kujipanyakulia ushindi katika jimbo la Puerto Rico na kubakiza kura 47 tu kufikisha kura elfu mbili 118 ili kushinda nafasi huiyo.

Watu wa karibu wa Obama wanaamini ya kwamba wiki hii itahitimisha safari ndefu ya mgombea wao kwa kupata ushindi na kuwa mgombea urais wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kwenye historia ya Marekani.

Hata hivyo kwa upande wake, seneta Hillary Clinton amesema atapambana mpaka dakika ya mwisho na kutupilia mbali hisia na wito wa kumtaka kung´atuka katika mbio hizo ambapo majimbo ya Montana na Dakota ya Kusini yatapiga kura zake kesho huku Obama akiwa anahitaji kura 45 ili kutangazwa mshindi.

Mgombea huyo ambaye ni mke wa rais wa zamani Bill Clinton anafanya hivyo kwa kile wachambuzi wa siasa za Democrat wanachokiona kuwa ni kumuwekea kauzibe Obama pale atakaposhinda amteue kuwa mgombea mwenza wa nafasi ya umakamu wa rais.

Akihutubia mkutano wa kampeni huko Dakota ya Kusini, Seneta Obama alimsifu mpinzani wake huyo akisema ni mchapakazi mzuri na hodari ambaye anaweza kuwa faida kubwa kwa chama hicho cha Democrat.

Kauli mbiu ya kampeni za Obama ni tunaamini katika mabadiliko, ndiyo tunaweza.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents