Michezo

USAJILI: Okwi kutua kifalme Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere (Picha+Video)

Katika kipindi hiki cha usajili wa wachezaji katika kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara na mashindano mengine, vita kubwa imeonekana kuelekea kwa watani wajadi ambao ni klabu ya Simba SC na Yanga katika kuhakikisha wanapata wachezaji bora wenye uwezo wa kuziletea manufaa timu hizo.

Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe alipo mkaribisha Okwi 

Baada ya filamu ya Ibrahim Ajib Migomba kumalizika kuzungumzwa midomoni mwa wapenzi wa soka nchini na riwaya tamu ya Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima kututupa kisogo hatimaye sasa ni tamthilia inayosubiriwa kwa hamu na mwadau pamoja na mashabiki wa soka inatarajia kuanza miuda si mrefu.

Hii ni kutokana na ujio wa mchezaji hatari Emmanuel Okwi ambaye pia mewahi kuichezea Simba katika vipindi viwili tofauti.

Jina la Okwi lilianza kutikisa soka la Bongo kuanzia Mei 6 ya mwaka 2012 tarehe 6 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya mchezaji huyo kutupia magoli mawili kati ya Matano ambayo time ya Simba waliyapata baad ya kuwafunga mahasimu wao wa jadi Yanga.

Shabiki wa Yanga akishangili klabu yake kumsajili mchezaji Emmanuel Okwi mwaka 2013

Katika ushindi huo mnono ambao Simba waliupata siku hiyo hawataweza kumsahau marehemu Patrick Mutesa Mafisango ambaye ndiye alipigilia msumari wa tano kwa njia ya penati katika ushindi huo.

Mchezaji Emmanuel Okwi akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo wao na Yanga mchezo ulimalizika na ushindi wa 5-0.

Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema mchezaji huyo Emmanuel Okwi atatua nchini kesho siku ya Jumamosi kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa kuiichezea tena Simba kwa mara nyingine ambao unatajwa kuwa wa miaka miwili.

https://www.facebook.com/baraka.adson/videos/1368597923255760/

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents