Michezo

Ole Gunnar kitu cha moto, Manchester United yapokea kipigo takatifu kutoka West Ham United, Rekodi zaendelea kuharibika

Ole Gunnar kitu cha moto, Manchester United yapokea kipigo takatifu kutoka West Ham United, Rekodi zaendelea kuharibika

Mikwaju ya Andriy Yarmolenko na Aaron Cresswell yameipatia West Ham ushindi wa pili nyumbani dhidi ya Manchester United, wanaosaia bila ya ushindi wa ligi ugenini tangu mwezi Februari.

Yarmolenko alifungua kwa bao la kwanza kunako dakika ya mwisho ya awamu ya kwanza ya mechi na kusukuam pasi kumpita David de Gea .

Cresswell aliisukuma timu hiyo ya Hammers pointi tatu mbele katika nusu ya pili kwa mkwaju muruwa.

Awamu ya kwanza ilionekana kuanza kwa kasi ndogo hususan kwa mashetani wekundu.

Juan Mataangeweza kusawazisha bao kwa wageni hao dakika mbili baada ya nusu ya pili ya mechi lakini akakosa kulilenga lango baada ya kupokea krosi nzuri ya chini kutoka kwa Andreas Pereira

Matokeo haya yanainua West Ham juu ya man United katika orodha ya ligi huku upande wa Ole Gunnar Solskjaer ukisalia na pointi tatu kutoka katika nafasi ya timu za juu.

Man United wafanikiwa kuondosha mkosi wa sare ya ugenini

Manchester United manager Ole Gunnar SolskjaerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mechi tatu zilizopita za ugenini za Manchester United katika ligi kuu ya England au Premier League ziliishia kwa sare ya 1-1.

Swali kubwa jioni hii lilikuwa ni je kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kitafanikiwa kuondosha mkosi huo wakati ikionana na West Ham united?

Jibu limekuwa ndio, walau kwa kushindwa 2-0 na timu hiyo ya Westham.

Westham ilishuka dimbani wakati ikimkosa beki wake wa kushoto Arthur Masuaku baada ya kutolewa katika mpambano dhidi ya Aston Villa.

Michail Antonio na Winston Reid wamekosekana kwa muda mrefu kwa timu hiyo ya Hammers.

Manchester United walikuwa na matumiani kuwa Daniel James atapona jeraha la mgongo alilopata huko Leicester wiki iliyopita

West Ham manager Manuel PellegriniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHuenda meneja wa West Ham Manuel Pellegrini akawa wa kwazna kuwashinda mameneha wanne tofuati wa Man United katika Premier League

Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba na Anthony Martial wote wamekosekana jioni hii, huku Luke Shaw nad Eric Bailly wakisalia nje pia kutokana na majeraha

Ulinganisho baina ya timu:

West Ham imeshinda mechi mbili kati ya zake nne za nyumbani dhidi ya Manchester United kwa uwingi wa ilizoshiriki katika mechi zake 19 za nyuma za nyumbani dhidi yao.

Manchester United imefunga magoli zaidi katika Premier League dhidi ya West Ham kuliko upande mwingine wowote.

Mashetani wekundu wameshindwa mechi mbili kati ya 21 za nyuma za ligi na kushindwa kufunga katika mechi hizo mbili tu.

Kauli za wakufunzi kuelekea mpambano?

Mkufunzi wa West Ham United Manuel Pellegrini: “Manchester United ilicheza Alhamisi usiku [katika Europa League] lakini ilibadili wachezaji 9, kwahivyo kitakuwa kikosi tofuati.

“Tupo katika wasaa mzuri, kwahivyo, iwapo tunacheza dhidi ya timu kubwa, ni lazima tuonyeshe tunaweza kucheza vivyo hivyo.”

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer: “mara ya mwisho [ushindi wa mnamo April wa 2-1 nyumbani dhidi ya West Ham] tulibahatika kuwafunga na utakuwa mtihani mzuri.

“Iwapo tutaendelea kujizatiti itakuwa rahisi kwa washambuliaji wetu, ambao watafahamu kwamba sio lazima tufunge mabao mawili mawili, au matatu matatu wakati wote.”

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents