Michezo

Tetesi za usajili barani Ulaya, Lukaku amsifi Conte huku Manchester ikiendelea kuyumba, Mourinho, Balotelli na wengine sokoni

Tetesi za usajili barani Ulaya, Lukaku amsifi Conte huku Manchester ikiendelea kuyumba, Mourinho, Balotelli na wengine sokoni

Kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona Xavi, ambaye ni meneja wa timu ya Qatari ya Al-Sadd, anasema kuwa itakuwa ni tatizo kwake kuwaongoza wachezaji wenzake wa zamani kama vile Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets katika Nou Camp. (Ara, via Goal)

Tottenham imetuma ujumbe kumchukunguza mchezaji wa kimataifa wa timu ya vijana waliochini ya miaka 21 wa Italia winga wa Fiorentina Riccardo Sottil ambaye ni mchezaji wa kiwango cha juu huku wakionyesha nia ya kumchukua kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 . (Express)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku anasema kuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ni mtu ambaye ''anamsaidia kila siku na humpa motisha''.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku anasema kuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ni mtu ambaye ”anamsaidia kila siku na humpa motisha”.

Matumaini ya Chelsea ya kusaini mkataba na mchezaji wa Napoli Elseid Hysaj msimu ujao yanaweza kugonga mwamba huku klabu hiyyo ya Italia ikiwa tayari kurefusha mkataba na kijana huyo kutoka Albania mwenye umri wa amiaka 25. (Express)

Meneja wa Everton Marco Silva ameutuma ujumbe umchunguze zaidi mshambuliaji wa timu ya RB Leipzig Yussuf Poulsen, mwenye umri wa miaka 25. (Express)

Roy Keane amesema kuwa "ameshtushwa na kusikitishwa " na namna klabu yake ya zamani Manchester United walivyoshindwa 2-0 na West Ham Jumapili
Image captionRoy Keane amesema kuwa “ameshtushwa na kusikitishwa ” na namna klabu yake ya zamani Manchester United walivyoshindwa 2-0 na West Ham Jumapili

Roy Keane amesema kuwa “ameshtushwa na kusikitishwa ” na namna klabu yake ya zamani Manchester United walivyoshindwa 2-0 na West Ham Jumapili. (Sky Sports, via Evening Standard)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 26, aliyejiunga na timu hiyo ya Italia kutoka Manchester United msimu huu, anasema kuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ni mtu ambaye ”anamsaidia kila siku na humpa motisha”. (Metro)

Mario Balotelli, anasema amefanya ''kazi kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopitaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES/AFP
Image captionMario Balotelli, anasema amefanya ”kazi kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita

Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anasema golikipa wa Uhispania David de Gea, mwenye umrui wa miaka 28, alikuwa na “bahati kidogo” kupata mkataba mpya mzuri na klabu hiyo . (Sky Sports, via Mail)

Mashabiki wapatao 1,000 wa timu ya Valencia waliandamana kabla ya mechi dhidi ya Leganes, kwa kutofurahishwa na namna mmiliki mwenza wa Salford City Peter Lim, na rais Anil Murthy anavyoendesha a klabu hiyo ya ligi ya La Liga . (Marca)

Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli,ambaye anaweza kuchezea Brescia dhidi ya Juventus Jumanne , anasema amefanya ”kazi kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita ” kuliko” kipindi cha muongo mzima wa kazi yake” huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 akilenga kupata nafasi katika kikosi cha nchi hiyo kitakachocheza kombe la Euro 2020. (Football Italia).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents