Burudani

Ommy Dimpoz: Sikualikwa ‘Zari All White Party ila sina tatizo na Diamond

Ommy Dimpoz hakuwa mmoja wa wasanii 100 walioalikwa kwenye ‘Zari All White Party’, Ijumaa hii.

Ommy

Kwa mujibu wa hitmaker huyo wa ‘Wanjera’, kunyimwa mwaliko wa kuhudhuria party hiyo hakumaanishi kuwa ana tatizo na Diamond.

Ommy alikuwa akihojiwa na kituo cha Radio 5 cha jijini Arusha weekend hii alipoulizwa kama amealikwa kwenye party hiyo.

“I am not invited,” alisema. “Lakini sina tatizo na Diamond, hajawahi kunikosea. Kikubwa ni kwamba amekuwa ni mfano kwa wasanii upcoming kwasababu hata mimi nimemkuta kwenye muziki na ni mmoja wa wanamuziki ambao walikuwa wananivuta hata mimi kuwa achana na mambo ya bendi na kuwa solo artist.”

Msikilize zaidi Ommy hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents