Omotola Jalade: Tanzanian Babes are hot!


Kuna mengi ambayo muigizaji wa filamu nchini Nigeria Omotola Jalade aliyekuja wiki hii kwaajili ya kumpa shavu Wema Sepetu kwenye uzinduzi wa filamu yake ya Super Star, ameondoka nayo kuwasilimua rafiki zake nchini Nigeria kuhusiana na alivyoiona Tanzania.
Ikiwa ndio mara yake ya kwanza kuja hapa nchini, bila shaka Omotola alifurahia sana safari yake nchini na kuondoka kichwani akiwa na mazuri na mabaya ya kusimulia kuhusu Bongo.
Hatuko interested hata hivyo kujua mabaya aliyoyaona sababu yatatuongezea tu stress zaidi.
Pamoja na yeye kuwa mrembo, diva huyo wa Nollywood amekiri kuwa Tanzania kuna ‘watoto wakali’.
Kupitia Twitter jana usiku alikuwa akiwamwagia sifa wasichana wa kitanzania kwa urembo wao kwa wafuasi wake zaidi ya 69,887 kwenye mtandao huo wa kijamii.
“Tanzanian Babes are Hot!” alitweet akiambatanisha na link ya blog ya Mange Kimambi iliyokuwa na picha za mashindano ya Miss Universe nchini Tanzania.
Hata hivyo muigizaji huyo ameondoka nchini bila kupata fursa ya kuzungumza na Rais Jakaya Kikwete kama ambavyo meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda alivyokuwa amepanga kufanya.
What went wrong? That’s a difficult question to be answered right now.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents