P-Funk Akanusha

P-Funk Akanusha
Producer maarufu na mmiliki wa studio za Bongo Records P-Funk aka
Majani ameibuka na kukanusha habari zilizozagaa mtaani siku za hivi
karibuni kuwa ameacha kusimamia wasanii wake wa siku nyingi Ferooz wa
Daz Nunda na Juma Nature

Akiongea na kituo kimoja cha Radio jijini Majani alisema ya kuwa hakuna ukweli wowote ule unaoendana na stori hizo za mtaani ya kuwa amewatosa wakali hao.

“Mimi sijawatosa kina Nature wale ni vichwa vyangu vya siku nyingi, kilichotokea ni kuwa sikuweza kuhudhuria uzinduzi wao kwasababu nilikuwa nje mkoani katika majukumu mengine ya kikazi pia” alisema Majani na baadaye ikajulikana kwamba alikuwa mikoani katika kutafuta washiriki wa Bongo Star Search 2009.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents