Burudani

P The Mc na Wakazi ‘wacharuka’, kisa?

Member wawili wa kundi la SSK, P the Mc na Wakazi wameeleza kushangazwa na utamaduni uliojengeka kwenye muziki wa Bongo Flava kuwa kuna video za kimataifa na za kawaida (local).

“International video ndio video zenye magorofa na magari makali?” alihoji P the Mc katika mahojiano na Bongo5.

“Nafikiri hili la kusema kuna video International na local ni dhana tu, kwa hiyo ni dhana ambazo huwa zinatengezwa ili zikae kwenye vichwa vya watu ila ukweli ni kwamba video ikiipanga katika matukio yaliyoongelewa kwenye wimbo tayari ni video kali haijalishi,” ameongeza.

Katika suala hilo rapper Wakazi naye amesema “video ya Dengue Fever ambayo nimeshoot ilikuwa nominated Kora Awards bajeti yake ilikuwa laki moja na nusu, mbona hizo na milioni 10 hajaingia katika nomination”.

P The Mc na Wakazi wamekutana katika ngoma kama ‘Habari ya Leo’ ya SSK na Amka Tanzania iliyokutanisha wasanii kama ZaiiD, Stereo, Nikki Mbishi, One The Incredible na Songa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents