Michezo

Picha: Chile yatwaa ubingwa wa Copa America

Michuano ya Copa America imefikia tamati leo hii kwa mabingwa watetezi Chile kuendeleza ubabe wake dhidi ya vigogo wa soka duniani Argentina.
Chile
Chile wakishangilia

Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikienda suluhu ya bila kufungana.

Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku ikushuhudiwa timu zote mbili zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji 10 baada ya Marcelo Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu dakika ya 28 kabla ya Marcos Rojo wa Argentina kutolewa nje dakika ya 43 kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Michuano imechukuliwa na Alexis Sanchez
Tuzo ya mchezaji bora wa michuano imechukuliwa na Alexis Sanchez

Katika upigaji wa penalti,Arturo Vidal wa Chile alianza kwa kukosa kabla ya Lionel Messi na Lucas Biglia kukosa kwa upande wa Argentina. Hii inakuwa fainali ya pili ndani ya miaka miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua ya fainali amapo mara zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju ya penalti.
Eduardo Vargas wa Chile na goli zake 6 amechukua Tuzo ya Mfungaji Bora wa Michuano Golden Boot
Eduardo Vargas wa Chile na goli zake 6 amechukua Tuzo ya Mfungaji Bora wa Michuano ‘Golden Boot’ . Kwa mara ya Pili mfululizo

Fainali hizi zilichezwa mwaka jana nchini Chile na kurudiwa mwaka huu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tokea kuanza kwa michuano hii mwaka 1916.

Tuzo ya Kipa Bora wa Michuano imeenda kwa Claudio Bravo
Tuzo ya Kipa Bora wa Michuano imeenda kwa Claudio Bravo wa Chile

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents