Moto Hauzimwi

Picha: Her Initiative ilivyotoa elimu kwa wanafunzi wa sekondari kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani

Taasisi ya HER INITIATIVE inayosaidia kuwaelimisha watoto wa kike kujitambua na kuishi bila kutegemea watu wengine pamoja na elimu ya upimaji afya, Alhamisi hii imetoa elimu hiyo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kawe iliyopo jijini Dar es Salaam katika kuhakikisha siku ya mtoto wa kike duniani inafanikiwa kwa asilimia kubwa.


Baadhi ya wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Kawe

Katika utoaji wa elimu hiyo ulihudhuriwa na Lydia Charles ambaye ni mwanzilishi wa taasisi hiyo na mtangazaji wa vipindi kutoka FEMINA, Shadee na Liliane Masuka (wote kutoka Clouds Media), Rio Paul pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi ya TAHMEF ambayo inashughulika na utoaji wa elimu ya afya.

Wakati huo huo taasisi hizo ziliweza kutoa baadhi ya misaada katika shule hiyo. Hizi ni picha za tukio hilo.


Mwanzilishi wa Her Initiative na mtangazaji wa vipindi Femina Lydia Charles (wa kwanza kulia) na Liliane Masuka kutoka katika kipindi cha The Storm cha Clouds TV (katikati) wakitambulishwa mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kawe


Mtangazaji wa Clouds TV katika kipindi cha Clouds E, Shadee akitoa somo kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Kawe


Baadhi ya viongozi wa taasisi ya TEHMEF wakitoa somo kwa wanafunzi

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW